MICHEZO
1 dk kusoma
Arsenal kuvaana na PSG nusu fainali ya kwanza
Timu ya Arsenal itakuwa katika uwanja wake wa nyumbani wakiwa wenyeji wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya mabingwa Ulaya tangu mwaka 2009. Jumanne usiku watapambana na Paris Saint-Germain.
Arsenal kuvaana na PSG nusu fainali ya kwanza
Timu ya Arsenal ikifanya mazoezi. /Reuters
tokea siku moja

Ushindi wa washika bunduki wa jumla ya magoli 5-1 dhidi ya mabingwa mara 15 Real Madrid umewapa fursa Arsenal kutinga nusu fainali, huku PSG ikipenya licha ya juhudi za Aston Villa kujaribu kupindua meza.

PSG si wageni katika hatua hii ya nusu fainali wamekuwepo katika nafasi hii kipindi cha miaka mitano iliopita, lakini wamefanikiwa kuingia fainali mara moja tu. Kama ilivyo kwa Arsenal, hata wao hawajawahi kushinda Ligi ya mabingwa Ulaya.

Baada ya kuendeleza matokeo mazuri hata nyumbani kwa Real Madrid Santiago Bernabeu, washika bunduki hao wamewafunga Ipswich 4-0 katika Ligi Kuu ya England na kupata sare dhidi ya Crystal Palace.

Wamesuwasuwa katika ligi ya nyumbani katika miezi michache iliopita na Liverpool tayari wameshachukua ubingwa siku ya Jumapili ikiwa bado mechi kadhaa kumaliza msimu.

Nusu fainali ya pili itakuwa wiki ijayo nyumbani kwa PSG.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us