AFRIKA
1 dk kusoma
Waziri Mkuu wa Libya aamuru kufungwa kwa balozi 25
Ofisi ya Waziri Mkuu inasema serikali itapitia upya kiwango cha wafanyakazi na mazingira ya kazi katika balozi zilizobaki.
Waziri Mkuu wa Libya aamuru kufungwa kwa balozi 25
Waziri Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah. / Getty Images
1 Mei 2025

Waziri Mkuu wa Libya Abdulhamid Dbeibeh siku ya Jumatano alitangaza mpango wa kufungwa kwa balozi 25 katika nchi mbalimbali kama hatua ya kupunguza matumizi ya serikali.

Uamuzi huo ni sehemu ya muendelezo wa hatua za kupunguza matumizi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Taarifa hiyo pia, imesema kuwa kutaundwa kwa kamati ya kuangalia na kutathmini kiwango cha watumishi na mazingira ya kazi katika balozi zilizosalia.

Serikali pia, imesitisha ufadhili mpya wa masomo katika nchi za kigeni na ufadhili wa sasa hautaendelea.

Fedha ambazo awali zilitengwa kwa ajili ya ufadhili wa masomo nje ya nchi hivi sasa zitaelekezwa kusaidia wanafunzi kufanya utafiti ndani ya Libya, pia kuendeleza mradi wa Maktaba ya Taifa ya Kielektroniki.

 

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us