AFRIKA
2 dk kusoma
Shambulio la RSF lauwa zaidi ya raia 41 na kujeruhi wengine katika eneo la El-Fasher, Sudan
Jeshi la Sudan limesema vikosi vyake vilizuia shambulio la RSF, na kuua wanamgambo 600
Shambulio la RSF lauwa zaidi ya raia 41 na kujeruhi wengine katika eneo la El-Fasher, Sudan
RSF yaendelea na mashambulizi yake dhidi ya raia wa Sudan / AA
29 Aprili 2025

Takriban raia 41 zaidi waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la makombora la na kikosi cha RSF huko El-Fasher, mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini magharibi mwa Sudan, jeshi la Sudan lilisema Jumanne.

Taarifa ya jeshi ilisema kuwa wanawake na watoto ni miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo lililolenga vitongoji vya makazi katika mji huo Jumatatu usiku. Jeshi limesema kuwa vikosi vyake vilifanikiwa kuzima shambulio la RSF katika mji huo na kuua wanamgambo 600 na kuharibu magari 25 ya kijeshi.

Hadi sasa hakuna tamko yoyote kutoka kwa kundi la waasi kuhusu taarifa hiyo ya kijeshi.

Mapigano yameendelea kati ya vikosi vya jeshi na wanamgambo wa RSF huko El-Fasher tangu Jumatatu, na kulazimisha mashirika ya kutoa misaada katika jiji hilo kusitisha usambazaji wake wa chakula kwa raia.

El-Fasher imeshuhudia mapigano makali kati ya jeshi la Sudan na RSF tangu Mei 2024, licha ya onyo la kimataifa juu ya hatari ya mapigano katika mji huo, ambao unatumika kama kitovu cha operesheni za kibinadamu katika majimbo yote matano ya Darfur.

Mapema mwezi huu, RSF ilidai kutwaa udhibiti wa kambi ya wakimbizi ya Zamzam mjini humo baada ya makabiliano na vikosi vya jeshi.

Janga la kibinadamu

Takriban raia 400 waliuawa, na karibu 400,000 walikimbia makazi yao kutokana na mapigano, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Tangu Aprili 15, 2023, RSF imekuwa ikipambana na jeshi la Sudan kudhibiti nchi, na kusababisha maelfu ya vifo na moja ya machafuko mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Zaidi ya watu 20,000 wameuawa hadi sasa, na wengine milioni 15 wamekimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa na mamlaka za mitaa.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us