AFRIKA
1 dk kusoma
Wanamgambo wa RSF washambulia Ikulu ya Rais mjini Khartoum
Wanamgambo hao wamekuwa katika mapigano na jeshi la nchi hiyo toka Aprili 2023, katika machafuko yalioua maelfu ya watu na kuwaacha wengine takribani milioni 13 bila makazi.
Wanamgambo wa RSF washambulia Ikulu ya Rais mjini Khartoum
Wanamgambo wa RSF. / Others
1 Mei 2025

Wanamgambo wa RSF wa nchini Sudan wameishambulia kwa mabomu Ikulu ya Rais mjini Khartoum, ikiwa ni tukio la pili ndani ya mji mkuu huo katika kipindi cha wiki moja.

Wanamgambo hao walitumia makombora ya masafa marefu katika shambulio hilo, toka waanza udhubiti wa mji mkuu wa Khartoum.

Kulingana na vyanzo vya kijeshi nchini humo, hakuna taarifa zozote za majeruhi na vifo kufuatia tukio hilo.

Wanamgambo hao wamekuwa katika mapigano na jeshi la nchi hiyo toka Aprili 2023, katika machafuko yalioua maelfu ya watu na kuwaacha wengine takribani milioni 13 bila makazi.

Siku ya Alhamisi, wanamgambo wa RSF walitangaza kutwaa jiji la El-Nuhud lililo Magharibi mwa jimbo la Kordofan.

Kulingana na mashuhuda, wanamgambo hao waliingia jijini humo mapema asubuhi wakitokea maeneo ya kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us