ULIMWENGU
2 dk kusoma
Ijue mamlaka ya Papa, Vatican
Vatican ni makazi rasmi ya Papa na imekuwa chini ya uongozi wa upapa tangu 1922.
Ijue mamlaka ya Papa, Vatican
Kivutio kikubwa vatican ni kanisa la St. Peter's Basilica / Reuters
tokea masaa 21

Huku Kanisa Katoliki likitarajia kumpata kiongozi mpya baada ya kifo cha Papa Francis, Vatican inangoja kiongozi mpya. Vatican ni mji na nchi, ambapo Papa, kiongozi wa Kanisa Katoliki huongoza.

Vatican ni makazi rasmi ya Papa, na imekuwa chini ya uongozi wa upapa tangu 1922. 

Papa hutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa nchi kupitia mamlaka aliyompa Rais wa Tume ya Kipapa ya Jimbo la Vatican, ambaye ameteuliwa na Papa kwa muda wa miaka mitano. 

Vatican ina vitengo vya sheria na bunge ambavyo vinaendeshwa na maafisa walioteuliwa na Papa. Lakini Vatican ni nchi tofauti na nyengine duniani. Kwanza Vatican iko ndani ya mipaka ya Roma Italy. 

Ina ukubwa wa hekta 44 tu, yaani unaweza kutembea nchi mzima kwa siku moja.

Idadi ya watu Vatican haifiki 1000, huku wengi wakiishi nje ya mji hasa Roma. Mapadre, makadinali na watawa wanachangia idadi kubwa ya wakazi. 

Mji wa Vatican hauna jela ila una seli chache kwa ajili ya watu kuwekwa kizuizini kabla ya kesi zao kusikilizwa.

Wale wanaopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo hutumikia kifungo katika magereza ya Italia kulingana na Mkataba wa Lateran.

Gharama za magereza zinalipwa na serikali ya Vatikani. 

Inalindwa na majeshi wa Uswisi.

Vatican haina hospitali, au muhimu zaidi, hakuna vyumba vya kujifungulia.

Kwa hiyo, hakuna mtu anayeweza kuwa raia wa Vatican kwa kuzaliwa.

Unapewa uraia tu kwa misingi ya kuteuliwa kufanya kazi katika nafasi fulani katika huduma ya kanisa. Uraia huo unatolewa kwa wanandoa, wazazi, na watu wengine wanaoishi pamoja.

Mara baada ya uteuzi kuisha, uraia huvuliwa. Kitaliano ndiyo lugha rasmi ya Vatican, na sarafiu yake rasmi ni Euro tangu 2002, hapo awali ilikuwa Lira ya Vatican. 

Kivutio kikubwa cha Vatican ni kanisa la St Peters Basilica, ambalo linaangaliwa kama kanisa kubwa la Kikatoliki duniani.

Mwaka wa 2025 Kanisa Katoliki linakadiria kupokea watalii milioni 32 watakaoitembea Vatican kwa sababu za kidini, na wengine kwa sababu ya kuona ubora wake wa kihistoria.

Mchakato wa kumpata papa mpya, kiongozi mpya wa Vatican, utaanza rasmi tarehe 7, mwezi Mei, 2025.


Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us