ULIMWENGU
1 dk kusoma
Kardinali Mtaliano ajiondoa mchakato wa kumpata mrithi wa Papa Francis
Mtaliano huyo, mwenye umri wa miaka 76 alihukumiwa na mahakama ya Vatican mwaka 2023 kwa ufujaji wa pesa, ulaghai na matumizi mabaya ya ofisi, katika kile kilichoitwa ‘kesi ya karne’.
Kardinali Mtaliano ajiondoa mchakato wa kumpata mrithi wa Papa Francis
Taarifa iliyotolewa na Kardinali Becciu, imesema kuwa imembidi afanye hivyo kama heshima kwa Papa Francis, japo alisisitiza kuwa alikuwa hana hatia./Getty / Getty Images
tokea masaa 21

Kardinali Giovanni Angelo Becciu amejiondoa rasmi kwenye mchakato wa kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani, kufuatia kifo cha Papa Francis, kilichotokea Aprili 21, 2025.

Mtaliano huyo, mwenye umri wa miaka 76 alihukumiwa na mahakama ya Vatican mwaka 2023 kwa ufujaji wa pesa, ulaghai na matumizi mabaya ya ofisi, katika kile kilichoitwa ‘kesi ya karne’.

Kabla ya maamuzi yake aliyoyafanya Jumanne ya Aprili 29, Kardinali Becciu alikuwa ameazimia kushiriki kwenye kongomano la kumchagua papa mpya, maarufu kama ‘Conclave’, ambao utaanza Mei 7, 2025.

Taarifa iliyotolewa na Kardinali Becciu, imesema kuwa imembidi afanye hivyo kama heshima kwa Papa Francis, japo alisisitiza kuwa alikuwa hana hatia.

“Nikiwa nimeliweka kanisa moyoni mwangu, ambalo nimelihudumia kwa imani na mapendo, na kwa kuheshimu umuhimu wa kongamano la Makardinali, imenibidi kuheshimu maamuzi ya Papa Francis ya kutokuingia kwenye kongamano hilo, japo sina hatia,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us