Kwaheri Papa Francis, ahsante kwa kuwajali Wapalestina
ULIMWENGU
4 dk kusoma
Kwaheri Papa Francis, ahsante kwa kuwajali WapalestinaKiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amefariki dunia Jumatatu ya Pasaka, wakati wakristu ulimwenguni wakiwa kwenye shamrashamra za kusherehekea ufufuko wa Yesu Kristo.
Wakati wa sinodi maalumu iliyofanyika Oktoba 2, 2024 mjini Roma, Papa Francis alitoa wito wa kufanyika kwa sala sala maalumu na mfungo, kama ishara ya kumbukumbu ya tukio lililoanzisha vita vya Gaza. / Reuters
21 Aprili 2025

Kiongozi Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amefariki dunia.

Kifo cha Papa huyo, ambaye ameshika hatamu ya Kanisa Katoliki toka Machi 13, 2013, kilitangazwa na kiongozi wa Makadinali, Kevin Farrel.

"Saa moja na dakika 35 leo asubuhi, Askofu wa Roma amerudi nyumbani kwa baba. Maisha yake yote alijitolea kwa huduma ya bwana na Kanisa lake yaliwekwa wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa lake," alisema katika taarifa yake.

Muargentina huyo atakumbukwa kwa misimamo yake ambayo, baadhi imeibua maswali, ikiwemo kupinga udhalimu wa kiuchumi, ubaguzi wa rangi, na matumizi mabaya ya kiiteknolojia.

Papa Francis amekuwa makini kushughulikia maeneo yenye migogoro ambayo yalionekana kupuuzwa na wasomi, wanasiasa na hata vyombo vya habari.

Jambo hilo limedhirika wazi kwenye mgogoro wa Gaza, ambako kwa namna ya pekee, Papa Francis ameonesha kusikitishwa na hali ya kuendelea kwa vita hivyo na zuio la kupeleka misaada eneo hilo pamoja na kusisitizia uharaka wa kidiplomasia kutatua jambo hilo akisema “Wapalestina na Waisraeli ni ndugu ambao wana haki ya kuishi kwa amani."

Akiwa anawaongoza Wakatoliki bilioni 1.41 ulimwenguni, Papa Francis alijiweka karibu na imani ya Kiislamu hususani alipoonesha haja ya kumaliza kwa mgogoro huo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 51, 200, wengi wakiwa wanawake na watoto.

Mara kwa mara, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amekemea uvamizi wa kijeshi uliofanywa na Israeli dhidi ya Wapalestina.

Katika siku za awali za vita hivyo, Papa Francis alitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano.

"Tafadhali tusitishe vita hivi," alisema, akiongeza kuwa vita hivyo vinasababisha sio vifo tu, bali mateso kwa watu wasio na hatia ."

Hata baada ya kutokea shambulio la anga lililofanywa kwenye Kanisa la Orthodox la huko Gaza, Oktoba 19, 2023, na kuua raia 18 wa Kipalestina waliokuwa wamejificha ndani yake, Papa Francis aliitaka Israeli ikomeshe vita hivyo kwa haraka.

Wakati wa sinodi maalumu iliyofanyika Oktoba 2, 2024 mjini Roma, Papa Francis alitoa wito wa kufanyika kwa sala sala maalumu na mfungo, kama ishara ya kumbukumbu ya tukio lililoanzisha vita vya Gaza.

Akizungumzia milipuko kwenye hospitali na shule, mwezi Disemba mwaka jana, Papa Francis alisema: "Huu ni ukatili, sio vita."

Pia aliwahi kuandika: "Kulingana na baadhi ya wataalamu, kinachotokea Gaza kinafikia sifa ya mauaji ya halaiki. Linapaswa kuchunguzwa kwa uangalifu ili kubaini kama inalingana na ikiwa inalingana na ufafanuzi uliotolewa na wanasheria na mashirika ya kimataifa."

"Daima, lazima ushinde vita! Lazima ushinde kila vita!"

"Nafikiria hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza ... nasisitiza ombi langu la kufunguliwa kwa misaada ya kibinadamu..."

Pia, alipata nafasi ya kuzungumzia shambulizi la anga la Disemba 17 huko Jabalia, ambalo liliua Wapalestina 25, wakiwemo watu 12 wa familia moja.

"Jana watoto walipigwa mabomu. Huu ni ukatili, hii sio vita," Papa aliwaambia wajumbe wa serikali ya Vatican.

"Na kwa uchungu, naifikiria Gaza, ukatili mwingi sana, wa watoto kupigwa risasi ovyo ovyo…ukatili ulioje," alisema Papa baada ya sala yake Malaika wa Bwana.

Siku chache baada ya mashambulizi ya Gaza, Papa Francis aliwapigia simu ya moja kwa moja na jumuiya ya Wakristo ambayo imekumbwa na kadhia ya mashambulizi ya Gaza.

Mazungumzo ya simu

Alifanya mazungumzo na Kanisa la Holy Family la huko Gaza, na kuwapa maneno ya kuwatia moyo pamoja na kuwakumbuka katika sala Wakristo na Waislamu waliojificha ndani ya kuta za kanisa hilo.

Parokia hiyo ya Holy Family ilikuwa imehifadhi watu wasiopungua 500, wakiwemo mapadre watatu, watawa watano na walemavu 58. Watu wengi waliojihifadhi katika parokia hiyo walikuwa ni Waislamu na watoto wanaohitaji uangalizi maalum.

Kulingana na Gabriel Romanelli, ambaye ni Paroko wa parokia ya Gaza, alisema kuwa watu wa eneo hilo walipata nguvu na kutiwa moyo zaidi baada ya simu hiyo.

Hata alipokuwa amelazwa hospitalini, akisumbuliwa na ugonjwa wa nimonia, Papa Francis aliendelea kuwasiliana na waumini wa kanisa hilo.

"Baba Mtakatifu aliwasiliana nasi siku mbili za kwanza baada ya kulazwa hospitalini, watu walikuwa wakisubiria hadi saa mbili jioni, licha ya kutokuwa na umeme katika eneo la Gaza,” alisema kiongozi wa Jumuiya ya Familia Takatifu, ambaye pia ni mzaliwa Argentina, Padre Gabriel Romanelli.

Pia alitumia wasaa huo kuwashukuru wananchi wa Gaza kwa maombi yao, wakati wa ugonjwa wake.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amefariki dunia Jumatatu ya Pasaka, wakati wakristu ulimwenguni wakiwa kwenye shamrashamra za kusherehekea ufufuko wa Yesu Kristo.

 

 

 

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us