29 Aprili 2025
Waziri wa mambo ya nje wa Brazil ametoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel kutoka Gaza wakati wa mkutano wa BRICS mjini Rio de Janeiro.
Kukusanyika kwa mawaziri wa mambo ya nje kutoka jumuiya ya BRICS - inayoongozwa na Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, na nchi nyingine - kunakuja kujibu hatua za upande mmoja zilizowekwa na Marekani na migogoro ya kimataifa inayoendelea.
Katika taarifa yake ya ufunguzi siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje Mauro Vieira alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Palestina akisema: "Kurejeshwa kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza na kuendelea kuzuia misaada ya kibinadamu ni jambo lisilokubalika. Kufeli kwa usitishaji mapigano uliotangazwa Januari 15 ni jambo la kusikitisha."